TUJUZANE BLOG

Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates

PAKUA APP YETU YA TUJUZANE

PAKUA APP YA TUJUZANE KUPATA NYIMBO MPYA IKO PLAY STORE

Saturday, December 12, 2020

NYOTA SABA WA SIMBA KUIKOSA MBEYA CITY KESHO, SOKOINE

 


KESHO Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.


Wachezaji saba watakosekana kwenye kikosi hicho kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimewafanya waweze kubaki Dar na wengine wapo nje ya Dar.

Thaddeo Lwanga kiungo mkabaji ndani ya Simba ikiwa ni ingizo jipya akiwa ni mchezaji huru licha ya kuanza mazoezi na timu bado hajapata nafasi ya kuwa kikosi cha kwanza mpaka pale usajili wake utakapokamilika dirisha dogo litakapofunguliwa Desemba 15.

Ibrahim Ajibu kiungo mshambuliaji, Charles Ilanfya mshambuliaji wa timu hiyo,Kennedy Juma beki wa kati na kiungo Bernard Morrison hawakusafiri na timu jana Desemba 11 kuelekea Mbeya.


Pia nyota Larry Bwalya raia wa Zambia huyu ana matatizo ya kifamilia akiwa zake nchini Zambia na anatarajiwa kurudi muda wowote na David Kameta beki wa kulia ambaye yupo na timu ya taifa ya chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ambayo imeweka kambi Saudi Arabia.