TUJUZANE BLOG

Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates

Friday, November 20, 2020

BREAKING NEWZ...Haruna Niyonzima Apata Ajali

 NYOTA wa kikosi cha Yanga, Haruna Niyonzima taarifa zinaeleza kuwa amepata ajali akiwa na mke wake nchini Rwanda wakati gari alilokuwa akiendesha kupata ajali wakati akimkwepa mwendesha baiskel katika eneo la Nyamata, wilaya ya Buswgwra.

 

Baada ya kumkwepa mwendesha baiskeli huyo alilivaa lori lililokuwa pembeni. Taarifa zinaeleza alikuwa na mke wake wa pili na hajapata majeraha mchezaji huyo anayeitumikia timu ya Yanga kwa Tanzania pamoja na timu yake ya Taifa ya Rwanda.

 

Mshauri wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha akizungumza na wanahabri leo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa Niyonzima hakuumia, yuko fiti na sasa uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa na anarejea kujiunga na Mabingwa hao wa Kihistoria katika ligi Kuu ya Tanzania Bara.

 

Niyonzima alikwenda kwao Rwanda kwa ajili ya majukumu ya kuitumikia Timu yake ya Taifa katika michuano ya kufuzu fainali za mashindano ya AFCON 2021.